BALOZI WA JAPANI NCHINI AAHIDI MAKUBWA MKOANI MARA
Barozi wa japan nchini Tanzania masaharu yoshida ametoa
msaada zaidi ya shilingi miamoja sabini kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu
pamoja nahuduma bora katika kituo cha
afya cha mrangi kilichopo wilayani musoma mkoani mara kwa ajili ya kujenga
nyumba za wauguzi na wafanyakazi,choo
cha wagonjwa shimo la kutupia kondo la nyuma na kurekebisha tanuru la kuchomea
taka za hospitalini kwa ajili ya kuwapa wagonjwa huduma safi na salama.
Ambapo utiaji saini wa mradi wa upanuzi wa kituo cha
afya cha murangi lengo nikuiwezesha
hospitali hiyo iliiwe na huduma
sitahiki ambapo kila mwananchi atahudumiwa
ipasavyo katika kituo hicho nakuondokana na adha ambayo walikuwa wakiipata kipindi cha nyuma kwa kupata huduma
katika hospitali ya mkoa ambapo niumbali mrefu kutoka katika kijiji hicho.
“Ninafuraha kubwa
na niheshima kwangu kusaini mkataba wa mradi huu mpya kupitia mfuko wa mpango
wa miradi midogo midogo kwa ajili ya
usalama wa binadamu”
Kituo hicho kilijengwa mwaka elfu moja mia tisa na
sabini na mbili kikiwa kituo kikubwa cha
afya na wagonjwa wengi wa rufaa hutoka zahanati nane wilayni hupelekwa katika
kituo hicho nakufanya kuwa na ugumu wa utoaji huduma ambapo vifaa tiba katika
kituo hicho hazijitoshelezi kutokana na idadi kubwa ya wananchi wanao hudumiwa katika
hospitali hiyo.
Pia alisema kuwa serikali ya japani imeihakikishia
serikali ya Tanzania itaendelea kutoa michango yake katika kusaidia mpango huo
wa upanuzi wa kituo hicho cha afya.
Naye mbunge wa musoma vijijini ambae pia niwaziri wa
nishati na madini profesa sospeter muhongo alisema kuwa mradi huo utachukua
mwaka mmoja kukamilika nahatimae
kukabidhiwa nakuupongeza ubalozi wa japani kwa ajili ya tiaji saini wa kiasi
cha pesa hicho kwani itasaidia katika utaoji wa huduma mbalimbali nchini
tanzania.
Aidha anarose nyamubi mkuu wawilaya ya butiama ambae pia
alimwakilisha mkuu wa mkoa wa mara aliwataka wananchi kukitumia kituo hicho kwa
ajili ya huduma nakuachanana natabia za kukimbia kwenda kwa waganga kwa ni
kituo hicho ndio suluhisho kwa wananchi wawilaya hiyo, wakati huo huo
mwenyekiti hali mashauri ya musoma vijijini pamoja na mkurugenzi wa halamshauri
ya musoma vijijin wali wataka wananchi kuachana naiasa ambazo hazina mbele wala
nyuma nakuwaunga mkono viongozi wanaotaka maendeleo nakuahidi kuulinda mradi
huo.
“Tunaahidi hakuna pesa itakayoliwa tutaurinda mradi huo
waziri wetu muhongo amekuwa tofauti na viongozi wengine yeye anawaleta viongozi
wenzake mnawaona nasisi tunasema hakuna hata senti itakayoliwa kwenye mradi
huu”alisema mwenyekiti
Wakati huo huo balozi huyo alitoa salam za pole kwa
tetemeko la ardhi kubwa lililokumba mkawa kagera ambapo alisema japani ipo
pamoja na Tanzania katika kipindi hiki kigumu huku aliahidi kuendelea
kusaidiana katika matatizo hayo.
kulia nui balozi wa japani nchini tanzania kushoto ni mkurugenzi musoma vijini wakionyesha mkataba
balozi akiwasili katika hospitali ya mlangi akisalimiana na viongoz wa vyama vya siasa