WANANCHI WA WILAYA YA HAI MKOANI KILIMANJARO WAZINDUA KAMPENI YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA MADARSA.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said mecky Sadiki akishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi,uchimbaji ulioenda sanjari na uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa, akishiriki kuchimba msingi kwa
ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi
iliyopo wilayani Hai.
Kaimu
Katibu Tawala wa wilaya ya Hai,Juliet Mushi akishiriki kuchimba msingi
kwa ajili ya ujenzo wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi
iliyopo wilayani Hai.
Baadhi
ya wananchi wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi
wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Msamadi.
Msingi
kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya
msingi Msamadi ukiwa umechimbwa na wananchi wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule zilizoko
wilaya ya Hai.
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki akizungumza wakati akizindua
rasmi kampeni za kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya
ya Hai.
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza na wananchi juu ya wazo
la kuanzishwa kwa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa
katika wilaya ya Hai.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia
fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa wakinyanyua mikono
kuashiria kuunga mkono kampeni hiyo.
Diwani
wa kata ya Masama Kusini Elingaya Masawe (Chadema) akizungumza wakati
wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa madarasa katika
shule za msingi na sekondari wilayani Hai.
Diwani
wa kata ya Bomang'ombe ,Joe Nkya (Chadema) akizungumza wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba
vya madarasa uliofanyika katika shule ya msingi Msamadi wilayani Hai.
Makamu
mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na Diwani wa kata ya Machame
Magharibi Goodluck Kimaro (Chadema) akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkuu
wa wilaya akizungumza namna wanavyoshirikiana na Madiwani wa upinzani
katika shughuli za menedeleoo ya wananchi wilayani Hai.kulia kwake ni
Diwani wa kata ya Masama Mashariki ,John Munis (Chadema).
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akitoa maelezo juu ya namna wananchi
watakavyo changia katika ujenzi wa madarasa kwa njia ya harambee ili
kupunguza changamoto ya vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Baadhi
ya wananchhi waliofika katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi
wa vyumba vya madarasa wakitoa ahadi zao wakati wa harambee ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo.
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiongoza harambee ya kuchangia
ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Msamadi iliyopo katika kijiji
cha kwa sadala.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport wakifuatilia matukio mbalimbali
yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba
vya madarasa.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Msamadi iliyopo kijiji cha Kwa Sadala wilayani Hai.
Mafundi
ujenzi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Said Mecky Sadiki pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport wakiwa katika picha ya pamoja na
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki pamoja na Mkuu wa wilaya
ya Hai, Gelasius Byakanwa mara baada ya kumalizika kwa harambee ya
kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo Swissport wametoa kiasi
cha Sh Mil 15.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.