Wanafunzi washindwa kumaliza Masomo Geita
SHUGHULI za Uchimbaji wa madini Katika wilaya na Mkoa wa Geita zimetajwa kuwa kikwazo katika sekta ya elimu kufuatia baadhi ya Vijana wa shule za Msingi na Sekondari kudaiwa kuacha masomo yao na kukimbilia kwenye Migodi kupata ajira kwa ajili ya kulisha familia zao.
Shughuli hizo zinadaiwa kuziathiri zaidi shule zinazomilikuwa na serikali kufuatia kubainika idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza na kidato cha kwanza kushindwa kushinda kumaliza masomo kwa kujiingiza kwenye shughuli hizo za uchimbaji.
Mratibu Elimu kata ya Nyankumbu Queen Mwamba ametoa kauli hiyo kwenye mahafali ya tatu ya shule ya Msingi Ukombozi yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa shule ya Sekondari ya Waschana Nyankumbu na kuhudhuriwa na wazazi na walezi pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Taasisis za Kifedha na elimu.
Awali mgeni rasimi Hassan Lugisha kwa niamba ya Meneja wa Benki ya NMB Mkoa wa Geita katika Hotuba yake amesema kuwa kwa wazazi kutoka sehemu moja kwenda nyingine si chanzo cha wanafunzi kuacha masomo yao huku mwenyekiti wa uwanja akiomba serikali kuwajengea uzio kwenye shule hiyo.
Wanafunzi hao walianza masomo ya darasa la kwanza mwaka 210 wakiwa 196 na waliomaliza darasa la saba ni 164 upungufu huo unatokana wengi wao kuolewa wakiwa wadogo na wengine kufanya kazi katika Shughuli za Uchimbaji wa madini.