Wadau wa sekta ya habari nchini wameiomba Serikali iwape muda wa kupitia na kutoa maoni Muswada wa huduma za kupata habari

 journalist-covering-event


Wadau wa sekta ya habari nchini wameiomba Serikali iwape muda wa kupitia na kutoa maoni juu ya Muswada wa huduma za kupata habari, kabla ya kujadiliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Muswada huo umeshawasilishwa Bungeni na Kamati ya Bunge tayari imeshakabidhiwa jukumu la kukusanya maoni ya wadau.

Ni mkutano wa dharula wa siku mbili Jijini Mwanza, ulioitishwa na Umoja wa Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC), kujadili baadhi ya mapendekezo yaliyopo ndani ya Muswada huo, yanayoonyesha kuwabana waandishi wa habari katika wajibu wao.
Akizungumzia Muswada huo mbele ya wadau wa sekta ya habari, Rais wa Umoja huo Deogratius Nsokolo, amesema Muswada huo ukipitishwa kama ulivyo bila wadau  kutoa maoni, Mazingira ya kazi za waandishi wa habari yataendelea kuwa magumu hapa nchini.
Katika mkutano huo Mkurugenzi wa (UTPC) Abubakar Karsan, amesema kutokana na ugumu wa kazi unaowakabili waandishi wa habari, ni vyema wadau wa habari wakajikita zaidi kutoa mapendekezo, yatayosaidia kurekebisha kasoro za Muswada huo.
Mapendekezo mengine yanayoendelea kujadiliwa ndani ya mkutano huo, ni kuangalia uwezekano ya uanzishwaji wa Chama cha wafanyakazi waandishi wa habari, ili kulinda maslahi yao, yanayodaiwa kutoendana na Mazingira ya ugumu wa kazi.
Powered by Blogger.