MAIKO WAMBURA AUNDA KAMATI



Chama cha soka mkoani Mara (FAM) kimeunda kamati ya watu sita kwaajili ya kusaidia timu ya polisi Mara kubadilishwa kutoka kuwa timu
inayomilikiwa na jeshi la polis na kuipeleka uraiani mabadiliko ambayo yatalenga kuifanya timu hiyo kupata ushirikiano mkubwa wa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Mara BW. MICHAEL RICHARD WAMBURA amesema kamati hiyo ya watu sita itajumuisha wajumbe watatu watatoka upande wa chama cha soka mkoa na watatu kutoka upande wa jeshi la polisi kamati ambayo itaanza kazi yake mara tu baada ya kupatiwa habibu za rejea.

Wambura amesema mbali na kamati hiyo kuwa na lengo la kubadili timu hiyo kutoka mikononi mwa jeshi la polisi lakini pia itasaidia kuweka mikakati thabiti ya kuipandisha timu hiyo ligi kuu soka Tanzania bara katika msimu ujao wa ligi.

Katika upande mwingine wambura amekabidhi mipira sita kwa mwenyekiti wa chama cha soka la wanawake ya mkoa wa Mara (TAWFA) ili kuongeza chachu ya mafanikio katika kuinua soka hilo mkoani hapa.

Akizungumza mara baada ya kupokea mipira hiyo mwenyekiti wa chama cha soka la wanawake mkoani Mara (TAWFA) BI. SOPHIA CHARLES amemshukuru mwenyekiti wa fam na kusema kuwa kitendo alichokionesha ni kweli kimeionesha thamani ya wananwake katika kuinua mchezo huo.



 KUSHOTO NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA MKOANI MARA MAIKO WAMBURA AKIMKABIDHI MIPIRA MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA WANA WAKE  MKOANI MARA BI SOPHIA CJARLES(TAWFA)

Powered by Blogger.