ALIYEKUWA KATIBU MKUU CHAMA CHA UDP AFARIKI DUNIA.

 
 
 
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha United Democratic Party UDP, John Nkolo, amefariki dunia akiwa nyumbani kwake Kibamba Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa UDP Taifa, John Cheyo, amesema msiba huo umetokea jana alfajiri baada ya marehemu kuugua kwa muda.

Amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu ambapo kesho kutwa Oktoba 13, mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kwenda Iramba mkoani Singida kwa ajili ya mazishi.

"Mwenyekiti wa Taifa wa United Demokratic Party (UDP) Mhe.John Momose Cheyo, anasikitika kuwajulisha viongozi, wanachama wa vyama vyote vya siasa nchini na Watanzania wote kuwa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa UDP BW.John Nkolo, alifariki dunia nyumbani kwake Mtaa wa Hoo Ndogo karibu na The Embassy of Heaven Ministry Kibamba Dar es salaam jana alfajiri". Imeeleza taarifa iliyotolewa na Cheyo hii leo.
Powered by Blogger.