Wakazi 552 wa vijiji vya Mgao na Kisiwa Mtwara wameitaka mamlaka ya bandari Tanzania ndani ya siku 15 kukamilisha walichodai

screen-shot-2016-10-11-at-4-56-06-pm
Wakazi 552 wa vijiji vya Mgao na Kisiwa  katika kata ya Naungu wilayani Mtwara vijijini wameitaka mamlaka ya bandari Tanzania  ndani ya siku 15 kukamilisha walichodai malipo ya fidia ya Ardhi yao iliyotwaliwa kupisha ujenzi wa bandari ya pili na kwamba endapo hilo halitatekelezwa watalazimika kudai haki yao mahakamani
.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye vijiji hivyo kwa nyakati tofauti tofauti, wakitawaliwa na jazba wananchi hao wanafikia hatua hiyo baada ya sintofahamu ya malipo yao kuendelea kutawala huku wakidai kushindwa kufanya shughuli yeyote ya maendeleo tangu serikali itwae maeneo hayo kisheria  mwaka 2015 .
Hata hivyo sintofahamu hii inawaacha njia panda wanakijiji hawa  baada ya maisha kuendelea kuwa magumu kila kukicha ambapo sasa wanamuomba rais John Magufuli kuingilia kati suala hili ili
waweze kulipwa fidia yao.
Baada ya taratibu zote za kutwaa eneo la kijiji cha Mgao na Kisiwa kukamilika kisheria na uthamini kufanyika kwa awamu mbili,  mamlaka ya bandari iliahidi kukamilisha malipo ya kiasi cha shilingi bilioni 12.2 kwa ajili ya heka 2500 walizozitwaa.
Powered by Blogger.