VIJANA NCHINI WANAPENDA KUJIAJIRI KULIKO KUAJIRIWA.
Imeelezwa
kuwa asilimia 50 ya vijana wanapenda kuanzisha biashara zao
ikilinganishwa na asilimia 25 ambao wangependa kuajiriwa kwenye taaluma
zao kama vile uhandisi, uanasheria, udaktari na ualimu
Akizungumza
jana Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa
vijana Tanzania, Mkurugezi wa Taasisi ya Afrika Mashariki ya Chuo
Kikuu cha Aga Khan, Alex Awet, alisema ripoti iliyohusisha vijana 1900
kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Tanzania inaonyesha matokeo
ambayo yanaleta matumaini na wasiwasi na haja ya kuchukua hatua za
haraka kwani baadhi ya matokeo ni kinyume na hali halisi inayofaa kuwepo
.
“Katika
mahojiano tuliofanya ni asilimia 20 tu ya vijana ambao walisema
wangependa kuwa wakulima huku walipoulizwa kuhusu wanachotathimini sana
asilimia 75 walitathimini imani katika dini kwanza,asilimia 61
walitathimini kazi kwanza na asilimia 46 walitathimini familia kwanza;
Inasikitisha
kuwa 75 ya vijana wa tanzania waogopa kudai haki zao kwa kuchelea
adhabu huku takiribani asilimia 45 wanaamini ufisadi una manufaa wakati
asilimia 58 wanaamini kuwa haijarishi nini vip mtu atatajirika kwa njia
zozote zile halali au halamu ,’’ alisema mkurugenzi huyo
Naibu
Waziri ofisi ya Waziri Mkuu, sera, bunge, kazi, vijana, ajira na
walemavu, Abdallah possi, alisitushwa na asilimia 44 ya vijana ambao
utafiti umebainisha wanaweza kupokea au kutoa rushwa.
“Utafiti
unaonyesha asilimia 75 wanaweza kuathiri au kujihusisha na udaganyifu
wakati wa kupiga kura huku ikiwa wazi kabisa asilimia 39 walisema
wangempigia kura mgombea aliyewahonga jambo ambalo siyo zuri na
tunatakiwa kukipinga kwa nguvu zote na kuwaomba vijana kutambua umuhimu
wa kulipa kodi kwani utafiti unaonyesha asilimia 34 pekee ya vijana
wanaamini kwa dhati kuwa ni muhimu kulipa ushuru,’’ alisema posi.