TAMWA yatoa semina ya uandishi wa habari za usalama barabarani kwa wanahabari Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kushoto) akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani jana katika ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda
Sanga akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanahabari juu ya
uandishi wa habari za usalama barabarani jana katika ofisi kuu ya TAMWA
Sinza jijini Dar es Salaam. Mwasilishaji
mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akiwasilisha mada kwa
waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za
usalama barabarani yanayofanyika kwa siku tatu kwenye Ofisi Kuu ya TAMWA
Sinza jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa watoa mada kutoka TAWLA akiwasilisha mada yake katika mafunzo
ya uandishi wa habari za usalama barabarani yanayofanyika kwa siku tatu
kwenye Ofisi Kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.
*****************************************
Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda
Sanga akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo alisema TAMWA ina
kila sababu ya kuingia katika mapambano ya ajali nchini kwa kuwa
zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa.
Alisema licha
ya ajali nyingi kupoteza maisha ya wanaume na kujeruhi wengine kundi
hilo limekuwa likiwaacha wake zao na watoto pasipo na msaada kwa kuwa
wengi humtegemea baba kama mtafutaji katika familia.
Alisema
wanawake wanaoachwa peke yao na familia wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa
wa familia jambo ambalo limeendelea kuwaingiza katika hali ngumu.
Aidha aliongeza
kuwa pamoja na hayo ajali nyingi za waendesha pikipiki maarufu kwa jina
la bodaboda zimekuwa zikiwaathiri akina dada na akina mama ambao ndio
watumiaji wa vyombo hivyo vya usafiri kiasi kikubwa.
Tamwa katika
mradi huo imejikita katika kutoa elimu ya madereva kuepuka ulevi,
ufungaji mikanda ya usalama katika magari, mwendo kasi na matumizi ya
kofia ngumu kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria wao.
Kwa upande
wake Mwasilishaji mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu alisema
suala la usalama barabarani si jukumu la taasisi moja hivyo kila mtu
anapaswa kushiriki katika kupambana na hatimaye kutokomeza ajali hizo
ambazo zimekuwa zikipoteza roho za watu, mali pamoja na kusababisha
ulemavu kwa baadhi ya waathirika wa ajali hizo.