Vifaa vya Utambuzi wa awali wa dawa za Kulevya na Kemikali bashirifu vyatolewa mipaka ya TUNDUMA


KATIKA kukabiliana na vitendo vya uingizaji na uvushaji wa dawa ya kulevya nchini,  hususani  maeneo ya mipakani na uwanja wa ndege, Tume ya kuratibu na Uthibiti wa dawa za kulevya nchini , kwa kushirikiana na Kitengo cha Polisi cha Kudhibiti dawa za kulevya Makao Makuu ADU, imetoa mafunzo kwa idara zinazohusika na mipaka na viwanja vya ndege katika mikoa ya Songwe na Mbeya, na kukabidhi vifaa vya utambuzi wa awali wa dawa za kulevya pamoja na kemikali bashirifu.

Mafunzo haya yametolewa Mjini Tunduma Mkoani Songwe  na  Aloyce Mathew Ngonyani, ambaye ni Mkemia Mwandamizi kutoka Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya, ambapo washiriki ni  jeshi la polisi kitengo cha kuzuia dawa za kulevya mipakani , idara ya uhamiaji , na Idara ya Forodha kutoka TRA,lengo ni  kuwawezesha kuwa na utambuzi wa awali wa dawa za kulevya pamoja na kemikali bashirifu.
Akikabidhi Vifaa hivyo ,Mihayo Msikhela  ambaye ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, na Mkuu wa Kitengo cha Kuthibiti na Kupambana na  Dawa za kulevya nchini anasema bangi ni kundi la dawa za kulevya ambalo linasumbua sana , na kwamba kwa kushirikiana kwa pamoja vita dhidi ya madawa ya kulevya inaweza kuisha kabisa ama kupungua kwa kiasi kikubwa.
Powered by Blogger.