Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameziagiza halmashauri zote nchini zilizopata fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa na vyoo katika shule za msingi zitumike kwa wakati badala ya kuchelewesha ujenzi huo kwa visingizio visivyo na msingi na hivyo kupelekea wanafunzi kuendelea kusoma katika mazingira magumu.

Prof.Ndalichako ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule za msingi,sekondari na vyuo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na Halmashauri na kubaini kuwapo kwa uzubaifu usiokuwa na sababu katika kuanza ujenzi wa miundombinu hiyo ikiwemo shule ya msingi Mbawala ambayo imepokea shilingi milioni miamoja na 91.8 lakini imeshindwa kuanza ujenzi wakati imepokea fedha hizo tangu mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumzia kuchelewa kuanza kwa ujenzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara  Omar Kipanga amesema sababu kubwa ya uchelewaji imetokana na ugumu wa kubomoa jengo chakavu
Mradi huo wa ujenzi wa miundombinu ya madarasa,vyoo na ukarabati wa majengo unafanyika katika baadhi ya halmashauri nchini umegharimu shilingi bilioni 14,wakati mkoa wa Mtwara umelenga katika shule tano na mpaka kukamilika kwake utagharimu shilingi milioni 868.
ndalichako-1Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako