NEC kuanza kufanya maboresho ya daftari la wapiga kura mwakani
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ifikapo mwaka wa fedha wa 2017/2018 kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2015.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati
akitoa elimu ya mpiga kura kupitia kipindi cha Alasiri Yetu
kinachorushwa na televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).
Alisema
kuwa baada ya uboreshaji huo wa mwaka 2017/2018, Tume hiyo inategemea
kuboresha kwa mara ya pili daftari hilo ifikapo mwaka wa fedha
2019/2020.
Bw.
Kailima alifafanua kuwa uboreshaji huo unafanyika kwa mujibu wa kifungu
namba 5 cha Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachoielekeza NEC
kuboresha daftari hilo mara mbili.
“Kwa
mujibu wa kifungu namba 5 cha Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
kinasema Tume ya Taifa ya Uchaguzi itapaswa kuboresha daftari la kudumu
la wapiga kura mara mbili, baada ya uchaguzi mara moja na kabla ya
uchaguzi ujao mara moja” alisema Bw. Kailima na kuongeza.
“Kwa
hiyo tumemaliza uchaguzi mwaka jana na kabla ya uchaguzi wa mwaka 2020,
Mungu akituweka hai tunategemea mwaka 2017/2018 tuboreshe daftari na
mwaka 2019/2020 tufanye hivyo”
Mbali
na kuzungumzia uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Bw.
Kailima aleleza jinsi tume hiyo inavyotekeleza mikakati ya kutoa elimu
ya mpiga kura na kwamba NEC itajipanga ili kwenda kutoa elimu hiyo
visiwani Zanzibar.
Alisema
NEC inapanga kwenda kutoa elimu hiyo kwenye Chuo Kikuu Zanzibar (State
University) mjini Unguja na baadaye kwenda kisiwani Pemba na pia
inategemea kushiriki Jitimai ili kutoa elimu ya mpiga kura kwa washiriki
wa mjumuiko huo.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi inaboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa
lengo la kuandikisha kila raia mwenye sifa za kupiga kura na kutunza
taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Inaelezwa
kuwa kuwepo kwa Daftari sahihi la Wapiga Kura linaloaminiwa na wadau ni
kigezo muhimu cha kufanikisha chaguzi huru, wazi, zenye kukubalika na
za haki zaidi.