TAKUKURU MKOANI MWANZA YAMNASA ASKARI FEKI WA JESHI LA WANANCHI JWTZ.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza, Ernest Makale, akitoa taarifa ya
kukamatwa kwa mwanamke aitwaye Felister Mathias Mawe, kwa tuhuma za
kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi
ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na jeshi
hilo kupitia maofisa anaofahamiana nao.
Makale ameeleza
kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kujipatia kiasi cha shilingi
240,000 kati ya shilingi 500,000 alizokuwa ameomba kutoka kwa mmoja wa
walioomba kujiunga na JWTZ.
Amebainisha
kwamba mtuhumiwa mmoja ambaye ni mstaafu wa JWTZ aitwaye Sophia Chacha
amekuwa akimsaidia mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa
wakihitaji kujiunga na jeshi ambapo ili kupata nafasi hiyo mtuhumiwa
amekuwa akihitaji kiasi cha shilingi 500,000.
Mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 10 mwaka huu katika hoteli moja iliyopo Kirumba Jijini Mwanza kufuatia mtego wa maofisa wa TAKUKURU.
"Kitendo cha
mtuhumiwa kujifanya afisa wa jeshi hakihusiani na makosa yaliyo chini ya
sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namaba 11/2007, hivyo jalada
lenye tuhuma hiyo namba PCCB/MZ/ENQ/40/2016 limehamishiwa kwa wakili wa
serikali mfawidhi ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani kujibu
tuhuma zinazomkabili". Alifafanua Makale.
Aidha Makale ameongeza kwamba
TAKUKURU wilayani Misungwi imemfikisha mahakamani Katibu wa Idara ya
Utumishi wa Waalimu TSD wilayani humo kwa kosa la tuhuma za kupokea
rushwa shilingi 400,000 kutoka kwa Kitoki Mgaya ili asimchukulie hatua
za kinidhamu kazini.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza, Ernest Makale, akitoa taarifa ya kwa
wanahabari kuhusu kukamatwa kwa mwanamke aitwaye Felister Mathias Mawe,
kwa tuhuma za kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua
fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya
kujiunga na JWTZ kupitia maofisa anaofahamiana nao.
Mtuhumiwa Felister Mathias Mawe,
anayetuhumiwa kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua
fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya
kujiunga na JWTZ.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo amekana
mashitaka hayo mbele ya wanahabari na kueleza kwamba alipokea fedha hizo
ili kumsaidia mtu aliyemtumia kufanya manunuzi ya nguo.
Kushoto ni mtuhumiwa Felister Mathias
Mawe, anayetuhumiwa kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na
kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata
nafasi ya kujiunga na JWTZ.
Kulia ni Sophia
Chacha ambaye ni mstaafu wa JWTZ anayetuhumiwa kumsaidia mtuhumiwa huyo
kwa kumuunganisha na watu waliokuwa wakihitaji kujiunga na JWTZ ambapo
hata hivyo amekana kuhusika na tuhuma hizo kwa madai kwamba hakuwa
akijua kama mtuhumiwa huyo amekuwa akipokea fedha kutoka kwa baadhi ya
watu hususani mabinti ili awasaidie kujiunga na jeshi la wananchi.
Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza