MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI BAADHI YA MAPINGAMIZI KWENYE KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA BUNDA MJINI.
Jaji wa Mahakama kuu Tanzania, Noel Chocha, leo ametupilia mbali pingamizi liliowekwa na wakili wa wajibu maombi, Cosntantine Mtalemwa, dhidi ya shaidi namba moja Ester Bulaya katika kesi namba moja ya mwaka 2015 ya uchaguzi wa wa jimbo la Bunda mjini mkoani Mara.
Kesi
hiyo ilianza kusikilizwa majira ya saa 7:00 mchana ambapo
Jaji Chocha alinza kutoa ufafanuzi dhidi ya mabishano ya hoja
yalijitokeza hapo octoba 12 mwaka huu kwa kueleza kile kilichosemwa na
mawakili wa pande zote mbili.
Baada
ya kuelezea melezo ya pande zote mbili Jaji huyo alisema amelikataa
pingamizi hilo kutoka na kanuni ya 23 ya uendeshaji wa mashauri ya
uchaguzi kama ilivyofanyiwa malekebisho mwaka 2015,ambayo haimkatazi
mjibu maombi kuleta au kutambulisha mambo mapya katika kiapo chake cha
ushahidi dhidi ya hati yake ya utetezi hakama mambo hayo hayakuainishwa
katika hati yake ya utetezi.
“Kufuatia
kupitia kesimbalimbali zilizokuwa zimeisha kutolewa
maamuzi yanayoendana kesi hii maamuzi ya Mahakama yamelikatta
pingamizi lilowekwa na walili Cosntantine Mtalemwa aneyewawakilisah
upande wa walalamikaji la kutaka vifungu namba 2,3,4,5,6,7 na 8
kuondolewa katika kiapo cha shahidi namba moja Estar Bulaya ambaye ni
mlalamikiwa, hayataondolewa na kiapo chake kitapokelewa bila kupunzwa
kitu chochote kwa mjibu wa kanuni ya 23 ya mwaka 2010,”alisema Jaji
Chocha.
Vile
vile kiapo chote cha shahidi Ester Bulaya kitaingia katika kumbukumbu
za Mahakama hivyo mtoa ushahidi ataulizwa maswali na mawakili wa
walalamikaji kwa upana zaidi kutokana na upana wa mabo yaliyopo
kwenye kiapo chenyewe ikiwemo mambo mapya aliyoongezeka kwenye kiapo
hicho.
Aidha
baada ya Jaji kumaliza kutoa maamuzi hayo, alizieleza pande zote mbili
kuwa yoyote ambaye ajalidhika na maamuzi hayo anaweza kukata
rufaa,akiihairisha kesi hiyo majira ya saa 8:45 mchana ikiwa na kutoa
maaelekezo kwa shahidi huyo ataanza kutoa ushahidi Octoba 17 mwaka huu
siji ya jumatatu.