SIMBA CEMENT YAZIPIGA TAFU SHULE TATU MKOANI TANGA.
KUFUATIA
Uhaba wa madawati katika shule za msingi halmashari ya jiji la Tanga na
wanafunzi kusomea chini, Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kimetoa
madawati 100 kwa shule tatu.
Shule hizo ambazo zimefaidika na mpango huo ni Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martini Shamba zote za halmashauri ya jiji la Tanga.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga , Thobias
Mwailapwa, Mkuu wa Idara Rasilimali watu kiwabda cha Saruji , Diana
Malambusi amesema msaada huo umekuja baada ya kuona kero ya wanafunzi
kusomea chini kutoisha.
Akizungumza
katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya, Thobias Mwailapwa,
amekishukuru kiwanda hicho (Simba Cement) na kuyataka mashirika na
taasisi pamoja na makampuni kuiga mfano huo ili kumaliza kero ya
wanafunzi kusomea chini.
Kwa
upande wake Afisa elimu shule ya msingi jiji , Khalifa Shemahonge,
amesema madawati hayo yatatumika kama inavyokusudiwa na kuahidi
kuyatunza ili kuongeza uelewa wa wanafunzi darasani.
Mkuu
wa Idara ya Rasilimali watu kiwanda cha Tanga Cement (Simba Cement),
Dianna Malambugi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga,
Thobias Mwailapwa, madawati 100 kwa shule tatu za msingi, Magaoni,
Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba za halmashauri ya jiji la Tanga
kupunguza uhaba wa madawati na wanafunzi kusomea chini.
Mkuu
wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, akimkabidhi Afisa Elimu Shule ya
Msingi halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa Shemahonge madawati 100
kwa shule tatu ya, Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba
yaliyotolewa na kiwanda cha Saruji cha Simba Cementi kupunguza uhaba wa
madawati kwa shule hizo.
Mkuu
wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa mwenye suti bluu (katikati) na
Afisa Elimu shule ya msingui halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa
Shemahonge (kulia) wakiwa na wafanyakazi wa kiwanda cha Simba Cement
mara baada ya makabidhiano ya madawati 100 kwa shule tatu za halmashauri
ya jiji la Tanga.
Walimu wa shule za
msingi Magaoni, Kiruku, Martin Shamba na Mkombozi wakiwa katika picha
ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga na wafanyakazi wa kiwanda cha
Saruji cha Simba Cement mara baada ya makabidhiano ya madawati 100 kwa
shule hizo.