CUF Kilwa yabariki Prof.Lipumba Kufukuzwa

piccuf
Sakata la mgogoro wa chama cha Wananchi CUF, linazidi kuchukua sura mpya, baada ya Kamati ya Utendaji ya chama hicho wilaya ya Kilwa kutoa tamko la kuunga mkono maamuzi yote yaliyokwisha chukuliwa na mamlaka halali za chama hicho kwa maana ya BARAZA KUU LA UONGOZI hivi karibuni kwa kuwasimamisha na kuwafukuza baadhi ya wanachama akiwemo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Prof.Ibrahim Lipumba
.
Tamko hilo limetolewa katika kikao maalum cha kamati hiyo kilichoketi chini ya Mwenyekiti wa Wilaya ya Kilwa katika mji mdogo wa Kilwa Kivinje, Selemani Bungara ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Selemani Bungara ambapo pia Katibu wa Jumuiya ya wanawake cuf Taifa Bi. Fatuma Omari Kalembo ambae hivi karibuni alivuliwa wadhifa huo na Prof Ibrahimu Lipumba kwa sababu za kiafya amewahakikishia wanachama wa chama hicho kutotambua maamuzi hayo yaliyokiuka sheria.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya wilaya hiyo akiwemo Mbunge wa Kilwa Kaskazni, Vedasto Ngombale pia wanazungumzia msimamo wa kamati hiyo.
Powered by Blogger.