Multichoice yafanya mapinduzi makubwa kupitia punguzo la bei za vifurushi
Multichoice
Tanzania imeamua kunufaisha wateja wake kwa kufanya mapinduzi makubwa
kupitia punguzo la bei na kuongeza chaneli 8 kupitia huduma yake ya
DStv. Huduma hizo mpya za punguzo la bei zitaanza rasmi kufanya kazi
kuanzia tarehe 1 Novemba, 2016. Vifurushi hivyo vya DStv ni DStv
Premium, Compact Plus, Compact, Family na Access. Punguzo hizo za bei ni
kama ifuatavyo:
DStv
Premium inapokea punguzo la asili mia 16%, kuanzia Novemba 1, na bei
itakuwa TZS 184 000. Pamoja na hayo, ongezeko la chaneli 8. DStv Compact
Plus, inapokea punguzo la asili mia 17%, na bei yake itakuwa TZS
122,500. Wateja wataendelea kufaidi burudani ya hali ya juu ya
vichekesho, tamthilia, sinema, michezo na vinginevyo.
Chaneli
hizo mpya zitakazorushwa ni Vuzu AMP, Lifetime, Discovery channel,Crime
& Investigation, History channel and Africa Magic Showcase. DStv
Compact Plus, imeongezewa chaneli za michezo zitakazoendeleza msisimko
kwa wapenzi wa mpira wa miguu kupitia vipindi vya UEFA Champions
Leagues, European Football leagues na Europa league. Hizo mechi zote
zinapatikana kwenye stesheni za SuperSport 6 (SS6) na SuperSport 4
(SS4).
Kwa
wapenzi wa filamu za kiafrika, watafaidi kupitia Nollywood , wapenzi wa
tamthilia zakilatino wataburudishwa na telenovelas pamoja na filamu za
Bollywood. Bila kusahau sinema zitakazopatikana kupitia chaneli za ROK, Eva Plus na B4U Movies.
DStv
Compact inapokea punguzo la asili mia 5%, na bei yake mpya ni TZS 82
250. Kifurushi hiki kina faida ya kurusha Premier League na La Liga
tangia mwanzoni mwa mwaka huu. Pamoja na hayo, wateja wa DStv
wataongezewa chaneli za ITV Choice (DStv chaneli 123), TCM (DStv chaneli
137) na SS4. Kuanzia Novemba na kuendelea, wateja wa Compact watafaidishwa na chaneli za ROK, Eva Plus na B4U Movies!
Kifurushi
cha DStv Family kimepokea punguzo la asili mia 16% na bei yake mpya ni
TZS 42 900. Kifurushi hichi kinapokea ongezeko la chaneli 5, ambazo ni B4U Movies, Eva, Eva Plus, SS4 na FOX.
Kifurushi cha DStv Bomba kitafaidisha wateja wake kwa ongezeko la
chaneli 3, na punguzo la asili mia 15%, bei yake mpya ni TZS 19,950.
Punguzo hili la bei kwa kifurushi hiki itaanzia tarehe 15 Novemba.
Katika
mkutano huo, Mkurugenzi Ronald Baraka Shelukindo alisema yafuatayo: Nia
yetu kuu katika kufanikisha punguzo hilo la bei ni kuweza kunufaisha
wateja wetu ili kuwapa huduma bora zaidi na kuthamini mchango wao katika
muendelezo wa kampuni yetu. Multichoice tunayo furaha kubwa pia
kuwaalika wateja wapya ili waweze kufaidi kupitia huduma zetu. Mapinduzi
haya ya punguzo za bei ni mwamko mkubwa sana katika kufanikisha malengo
yetu sio tu hapa nchini, lakini Afrika nzima.