Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Nchini umepunguza idadi ya utoro mashuleni.
Serikali kupitia mpango wa kuinua ubora wa Elimu Tanzania
(Education Quality Improvement
Programme Tanzania- EQUIP-T) umepunguza kiwango cha utoro na idadi ya
wanafunzi wasiojuakusoma na kuandika shule za Msingi mkoani Dodoma.
Hayo yamesemwa leo, Mjini Dodoma
na Kiongozi wa mpango huo Mkoa wa Dodoma Francis Liboy katika semina
ya mawasiliano ngazi ya Wilaya na jinsi ya kupashana simulizi ya
mabadiliko iliooandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na
EQIP-T.
“Mradi wa EQUIP-T umewezesha
walimu shule za msingi kupata mafunzo mbalimbali ya njia bora ya
ufundishaji kea wanafunzi wa madarasa ya Awali mpaka darasa la Nne kujua
kusoma,kuandika na kuhesabu kwa ufasaha na kwa muda mfupi,” alifafanua
Liboy.
Kutokana na mafunzo hayo kwa walimu idadi ya wanafunzi
wasiojua kusoma, kuandika na
kuhesabu imepungua kwa kiasi kikubwa kwa mkoa wa Dodoma na wilaya zake
kutokana na walimu kuwa na mbinu mbalimbali za ufundishaji.
Mpango huo pia umeweza kuifanya jamii kuona shule ni mali
yao hivyo jamii imekuwa mstali wa mbele kufuatilia
mahudhurio ya watoto wao hivyo kupunnguza utoro kwa
kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Wilaya ya
Mpwapwa Anderson Njolegwa amesema
kuwa mpango huo umeweza kupunguza utoro katika Wilaya hiyo kutoka
wanafunzi 828 mwaka 2013 mpaka wanafunzi 572 mwaka 2016 ambao
wanaendelea kupungua kila siku.
Mpango wa EQUIP-T ni mpango wa miaka minne ambao
ulianza mwaka 2014 ukiwa na dhamira ya kuinua ubora wa
Elimu Nchini ambapo mpaka sasa mpango huo upo katika mikoa ya Dodoma, Kigoma, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mara na Lindi.