Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni
Kibamba, akihojiwa na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, kuhusiana na
sakata la Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza kugoma kukabidhi
mihuri yao ya utendaji kazi.
"Hii mihuri ya
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ni dili, hivyo haitambuliki kwa sasa,
kwanza imesababisha migogoro mingi kwa wananchi ikiwemo uuzaji wa
viwanja kiholela". Amesisitiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni
Kibamba.
Ameshikilia
msimamo wake kwamba mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini
Mwanza haitambuliki kama awali alivyosema kwamba waikabidhi ofisini
kwake.
Leo Wenyeviti
wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza wameendelea kushikilia msimamo wao wa
kutorudisha mihuri hiyo huku wakitishia kutoshirikiana na Watendaji
Jijini Mwanza.
Juzi jumamosi
Wenyeviti 174 wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza, walivunja kikao na
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, baada ya Mkurugenzi huyo kuwataka
kukabidhi mihuri yao.