Baada ya Maadhimisho ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama Barabarani kufanyika Kitaifa mkoani Geita kuanzia Septemba
29 hadi Oktoba Mosi Mwaka huu, Maadhimisho kama hayo kwa mkoa wa Mwanza
yamezinduliwa hii leo kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza ambapo
imeelezwa kwamba bado juhudi za kila mtumiaji wa barabara zinahitajika
ili kutokomeza ajali za barabarani.
Kamanda
wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein,
amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwaka jana kati ya mwezi januari na
septemba kulikuwa na ajali 161 zilizosababisha vifo 132 na majeruhi 187
na kwamba kwa kipindi kama hicho mwaka huu kulikuwa na ajali 159
zilizosababisha vifo 150 na majeruhi 162 ambapo takwimu hizo zinaonesha
kuwepo kwa ongezeko la vifo 18 sawa na asilimia 12 na upungufu wa
majeruhi 25 sawa na asilimia 13.3
Pichani juu ni maandamano ya bodaboda
pamoja na wa watumiaji wengine wa
barabara yakiingia Uwanjani kwenye
maadhimisho hayo ambayo yamezinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John
Mongella.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza
Kamanda
wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein,
akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza
Viongozi mbalimbali mkoani Mwanza
Baadhi ya maofisa wa polisi mkoani Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella
(kushoto) akiteta jambo na Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed
Msangi (kulia) kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary
Tesha (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonald
Massale (kulia) kwenye uzinduzi huo.
Mwanahabari Simba Kabonga wa Barmedas Tv akipokea cheti cha utambuzi wa kampuni hiyo katika kutoa elimu ya usalama barabarani
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa
Waendesha Bodaboda mkoani Mwanza, Seifu Kagoma, akionesha cheti cha
utambuzi kwa taasisi hiyo kutoka kwa Kamati ya usalama barabarani mkoani
Mwanza.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Butimba
Jijini Mwanza wakiingia uwanjani kuimba wimbo wa kuhamasisha matumizi
sahihi na salama ya barabarani.
Askari wa usalama barabarani mkoani
Mwanza, wakitoa elimu ya usalama barabarani kwa baadhi ya wananchi
waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoani
Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa
Mwanza, John Mongella, amewataka watumiaji wa barabara mkoani Mwanza,
kuzingatia sheria za usalama barabarani jambo ambalo litasaidia juhudi
za kupambana na ajali kufanikiwa.
Mongella ametoa
kauli hiyo hii leo kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani mkoani Mwanza, uliofanyika katika Uwanja wa Furahisha
Jijini Mwanza, ambapo elimu ya usalama barabarani itaendelea kutolewa
kwenye maadhimisho hayo kwa juma zima.
Amesema
watumiaji wote wa barabara wanao wajibu wa kufuata sheria za usalama
barabarani huku akikemea tabia ya baadhi ya abiria wanaowahimiza
madereva kuendesha vyombo vyao kwa mwendo kasi.
Kamanda wa
Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein, amebainisha
kwamba kwa kipindi cha mwaka jana kati ya mwezi januari na septemba
kulikuwa na ajali 161 zilizosababisha vifo 132 na majeruhi 187 na kwamba
kwa kipindi kama hicho mwaka huu kulikuwa na ajali 159 zilizosababisha
vifo 150 na majeruhi 162 ambapo takwimu hizo zinaonesha kuwepo kwa
ongezeko la vifo 18 sawa na asilimia 12 na upungufu wa majeruhi 25 sawa
na asilimia 13.3
Akizungumza kwa
niaba ya watumiaji wa barabara, Makamu Mwenyekiti wa Waendesha bodaboda
mkoani Mwanza, Seifu Kagoma, amesema kila mtumiaji wa barabara anao
wajibu wa kuwa na tahahadhali awapo barabarani badala ya kusubiri wajibu
huo kutoka kwa mwenzake.
Maadhimisho ya
wiki ya usalama barabarani hufanyika kila mwaka nchini lengo likiwa ni
kutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya barabara kwa makundi yote ya
watumiaji wa barabara ambapo mwaka huu kitaifa yalifanyika mkoani Geita
kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba Mosi ambapo kauli mbiu yake ni
“Hatutaki ajali, tunataka kuishi salama”.