January Makamba : Kuna haja ya kuboresha sheria ya mazingira ya mwaka 2006

ccmresultspic
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira January Makamba amesema bado kuna haja ya kuboresha sheria ya mazingira ya mwaka 2006 sheria ambayo inaonekana kuwa na mapungufu katika vipengele kadhaa.

Makamba ameyasema hayo wakati akifungua warsha hiyo waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira January Makamba amesema sheria iliyopo bado inahitaji kufanyiwa marekebisho ambayo yatasaidia kutoa minya ya wawekezaji kuweza kuwekeza katika maeneo yenye fukwe ili kuziweka fukwe hizo katika madhari nzuri inayofaa.
Aidha Makamba amesema bado kuna uhitaji mkubwa kwa wananchi kuweza kuhifadhi vyanzo vya mito pamoja na fukwe kwa sasa zinaonekana kuwa na hali ambayo hailidhishi .
Kwa wao waandaaji wa warsha hiyo ya siku mbili ambao ni baraza la hifadhi wa mazingira Nemc wamesema wameamua kuandaa warsha hiyo kwa lengo la kuwakutanisha wadau hao ili kutoa mapendekezo yao ambayo yatawasilishwa katika wizara husika na kuyafanyia kazi ili kuboresha sheria hiyo ya mazingira.
Wadau wa masuala ya mazingira kutoka mikoa mbalimbali nchini leo wamekutana jijini Dar es salaam kujadiliana juu ya sheria ya mazingira ya mwaka 2006 sheria ambayo imeonekana kuwa na mapungufu ikiwemo kutokutoa uhuru kwa wawekezaji katika kuwekeza katika fukwe mbalimbali nchini.
Powered by Blogger.