Maafisa manunuzi na mashuhuri wa serikali wanakabiliwa na changamoto kutojua taratibu za kutumia EFD’s





 screen-shot-2016-10-06-at-2-35-37-pm


Miongoni mwa changamoto hizo ni utekelezaji wa kodi ya zuio ambayo wakati serikali inapotoa malipo kwa watoa huduma kuna kiasi cha fedha kinachopaswa kuzuiwa kikiwa ni sehemu ya kodi na kuiwasilisha serikalini, lakini wakati mwingine imekuwa haifanyiki hivyo kutokana na maafisa hao kutoelewa vyema sheria hiyo, hivyo kuwajibika kuilipa pamoja na adhabu pale wanapobainika.

Naibu Kamishna wa kodi za ndani TRA, Abdul Zuberi, anasema baada ya kugundua baadhi ya mazuio hayakatwi au hayawasilishwi TRA wameunda mkakati wa kuwatambua ili kuwezesha mamlaka kuwafuata na kuhakikisha kodi ya serikali inakusanywa, huku wakijikita kuwafikia maafisa wa serikali nchini kwa kuwaelimisha namna ya kuzuia kodi hiyo na jinsi ya kuiwasilisha TRA kwa wakati.
Jana Mamlaka ya mapato Tanzania ilifanikiwa kukutana na maafisa 200 wa idara za serikali ambapo leo imeendelea na mafunzo kwa maofisa wengine 200, zoezi ambalo ni endelevu kwa wadau wote wa kodi nchini likilenga kuhakikisha mamlaka inafikia malengo ya serikali ya ukusanyaji wa mapato. Serikali ya awamu ya tano imelenga kuwa na bajeti inayojitegemea badala ya kutegemea wafadhili.
Powered by Blogger.