Mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa tumbo arudi Ghana salama
Mtoto mmoja kutoka Ghana ambaye
alizaliwa viungo vyake vya tumbo vikiwa nje amerudi nyumbani baada ya
kufanyiwa upasuaji nchini Uingereza.
Mnamo mwezi Juali iliripotiwa kwamba mtoto mwenye umri wa miaka 3 Ethan Suglo alisafiri hadi nchini Uingereza baada ya fedha kuchangishwa ili kumwezesha kufanyiwa upasuaji huo wa kuokoa maisha yake.
Baada ya upasuaji uliofanikiwa wanahabari ilikuwa hapo kumuona mtoto huyo akikutanishwa na familia yake baada ya kurudi nchini Ghana.