Jumuiya ya Vijana CUF wamemtaka Maalim Seif kukinusuru chama hicho

Jumuiya ya Vijana ya Chama cha wananchi CUF kutoka wilaya tatu za Mkoa wa Dsm wamemtaka M/kiti wa Chama cha wananchi Cuf pamoja Maalim Seif Sharifu Hamad kukinusuru chama hicho kwa kukutana na Kuzungumza pamoja ili kumaliza mpasuko unaoendelea kukigawa chama hicho bara na Visiwani.
Aidha Umoja huo umezitaka pande hasimu kuacha kutumia lugha zisizo na Staha dhidi ya Viongozi wa juu wa chama hicho kwa kuwa zinaweza kueneza Chuki lakini pia kuchochea Ubaguzi kati ya wafuasi wa Tanzania bara na Visiwani.
M/kiti wa Juvi-CUF wilaya ya Ilala Canal Ali Shaghary amesema Jumuiya hiyo inasikitishwa na mwenendo unaendelea wa msuguano ndani ya chama hicho.

Powered by Blogger.