Serikali yaendelea kuandaa wazawa kusimamia Gesi asilia

 6
Serikali imeendelea kuchukua hatua kadhaa za kuhakikisha inajenga uwezo wa rasilimali watu yenye ujuzi, watakaoweza kusimamia na kuendesha miundombinu ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara na Songo Songo hadi Dar es Salaam kupitia Somanga,bomba lenye urefu wa kilometa 548.

Miundo mbinu hiyo iliyogharimu  dola za kimarekani bilioni 1.53 sawa na trillion 2.926 za kitanzania, inatumika kusafirishia gesi asilia hadi jijini Dar es salaam,  asilimia 95 ya gharama hizo zinatokana na mkopo kutoka Benki ya Exim ya China huku asilimia 5 ikitoka serikalini.
Ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuzinduliwa kwa miundo mbinu ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara na Songo Songo hadi Dar es Salaam
Mshauri mkuu na wakandarasi wa mradi huo wamesema kwa sasa kwa kushirikiana na serikali wameendelea kusomesha watanzania ili kuhakikisha wanasimamia mradi huo mkubwa  wa gesi asilia.
Leo Mshauri Mkuu wa mradi huo, Kampuni ya Afrika Kusini ya Worley Parsons imekabidhi rasmi kwa serikali kazi yake, na kuuelezea kuwa mradi huo ni moja ya mradi mkubwa uliotekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.
miundombinu uchakata na kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara na Songo Songo hadi Dar es Salaam Itakuwa na uwezo wa kusukuma futi za ujazo milioni 784 kwa siku ifikapo mwaka 2020, na inatarajiwa kudumu kwa takriban miaka 50 kabla ya kuanza kuifanyia matengenezo.
Powered by Blogger.