Halmashauri ya Handeni na Kilindi zamaliza mgogoro wa mpaka na Mwekezaji
Viongozi
wa halamshauri ya wilaya ya Handeni na Kilindi wamefanya ziara ya
kwenda kutatua mgogoro wa mpaka wa kijiji cha Gole kilichopo wilayani
Handeni na Negelo kilichopo wilayani kilindi.
Ziara
hiyo iliofanyika mwishoni mwa wiki Oktoba 8,2016,imefamyika kufuatia
kijiji cha Gole kulalamika kuwa kuna muwekezaji anafanya shughuli za
kilimo na ufugaji katika eneo la hifadhi ya msitu wa kijiji uliotengwa
tangu 2011.
Wakuu
wa wilaya ya Handeni na Kilindi sambamba na Wakurugenzi wa wilaya hizo
walifika eneo la mgogoro huo wakishirikiana na wataalamu kutoka pande
zote mbili,na kusoma ramani iliyotumika kutenganisha mipaka ya wilaya na
vijiji.
Mgogoro
ulimalizika baada ya wataalamu hao wa mambo ya ramani, kutoa umiliki
halali wa eneo aliyopo muwekezaji kuwa ni ndani ya Kijiji cha
Gole.Wataalamu hao walieleza kuwa Sheria,taratibu na kanuni zitafuatwa
katika kumuondoa muwekezaji huyo katika eneo hilo la hifadhi ili aweze
kufanya shughuli zake za kiuchumi katika eneo husika kulingana na mpango
bora wa ardhi.
Aidha
uongozi uliwataka wataalamu wa pande zote mbili kukaa ndani ya siku
kumi kuanisha mipaka inayotenganisha vijiji vya wilaya ya Kilindi na
Handeni ili kuondoa utata kwenye vijiji vingine vilivyo na utata.