Taarifa ya Yanga kuhusu kumtimua kazi Kocha Hans Van De Plujin na Juma Mwambusi
Kumekuwepo
na taarifa katika mitandao mbalimbali ambayo inaihusisha klabu ya Yanga
kumfukza kazi kocha mkuu wa klabu hiyo, Hans Van De Plujin na msaidizi
wake, Juma Mwambusi.
Taarifa
hizo zimeufikia uongozi wa Yanga na kupitia ukurasa wa klabu hiyo wa
Facebook umetoa taarifa ya kukanusha kumfukuza kocha na kwamba Plujin
bado anaendelea na kibarua chake kama kawaida.
Press Release
Klabu ya Yanga inapenda kuwatangazia wanachama wote wa Young Africans Sports Club (YANGA) kuwa habari zilizoenea kwenye mitandao na magazeti juu ya mabadiliko ya benchi la ufundi wa klabu kuwa ni uzushi na sio za kweli.
Uongozi bado unamtambua Mwalimu Hans Van De Plujin kama kocha mkuu na Juma Mwambusi kama kocha msaidizi.
Uongozi unawaomba wanachama kupuuzia hizo habari popote pale wanapokutana nazo.
'YANGA DA