DC STAKI ASIMAMIA ZOEZI LA KUCHOMA SHAMBA LILILOLIMWA MIRUNGI
Wakazi wa Kijiji cha Kisesa Kata ya Vudee wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa shambala Mirungi
Mkulima
wa zao la Mirungi Johnson Charles Kangara akiwa ameshika mafuta ya taa
tayari kwa ajili ya kuteketeza shamba lake la Mirungi
Shamba la Mirungi likiteketea baada ya agizo la Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki
Dc Staki akiwasisitiza wananchi kutojihusisha na kilimo cha zao la Mirungi
Mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka
huu Uongozi wa Wilaya ya Same ulitangaza vita dhidi ya wakulima wa
Bangi, na Mirungi huku akitangaza kuwa kifungo cha miaka 30 kitawahusu
wakulima wote wanaojishughulisha na kilimo hicho haramu kwani Bangi na
Mirungi ni hatari kwa afya za watumiaji na kuisababishia serikali hasara
kwa kutopokea Kodi.
Kiama hicho kilitangazwa na Mkuu
wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule wakati akikabidhiwa mradi
wa Ruvu muungano uliojumuisha zahanati sita, Nyumba mbili za waganga,
matanki saba ya kuvuna maji na madarasa 54, ofisi 16 za walimu, vyumba
na vyoo vya chuo cha ufundi makanya uliofadhiliwa na shirika la World
Vision Tanzania.
Dc Staki alisema kuwa kwa
asilimia kubwa serikali imekuwa ikiwadhibu wanaoingiza Mirungi na Bangi
sokoni huku ikiwasahau kuwachukulia hatua wale wote wanalima zao hilo.
Hivi karibu katika kijiji cha kisesa kata ya Vudee Wilayani
humo ilibainika kuwa kuna wakulima wa Mirungi ambao wanajihusisha na zao
hilo kwa muda mrefu pasina serikali kuwabaini na kuwa sugu kwa kilimo
hicho hatimaye kukiona kama kilimo cha halali.Dc Staki alipotangaza
kiama cha kukabiliana na wale wote wanaojihusisha na kilimo hicho
aliahidi kuwatafuta wakulima hao na hatimaye kuwachukulia hatua za
kisheria na kuhakikisha kuwa Wilaya ya same inakuwa safi pasina kuwa na
Mirungi.
Hata hivyo katika ziara yake ya kazi Mhe Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki alipozuru kijiji cha kisesa kata ya Vudee alifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mkulima wa zao la Mirungi Johnson Charles Kangara na hatimaye kumuelekeza kuwasha kiberiti yeye mwenyewe katika shamba zima na kuchoma zao hilo.
Dc Staki ameahidi kuhakikisha Wilaya ya Same inasifika kwa kilimo cha mazao mengine rafiki katika jamii ya Biashara na chakula na kuteketeza mazao yote haramu.