BENK ya CRDB tawi la Musoma,imetoa misaada mbalimbali ya kijamii katika gereza la Musoma katika kuazimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo meneja wa benki hiyo Wilfred Masawe,akidai kila mwaka wanapokuwa wakiadhimisha wiki hiyo wamekuwa wakifanya matukio tofauti ya kusaidia jamii na safari hii walilenga kusaidia wafungwa na mahabusu waliopo gerezani kwa kuwa nao ni sehemu ya jamii.
Maafisa wa benki ya CRDB wakishusha bidhaa mbalimbali walizokwenda kuwasaidia wafungwa
Sembe chapa nguvu ikishushwa kwaajili ya kukabidhi kwa viongozi wa gereza la Musoma
Meneja wa benki ya CRDB tawi la Musoma,Wilfred Masawe(kushoto)akimkabidhi sehemu ya msaada mkuu wa gereza la Musoma,Humba Humba,huku askari wa magereza na maafisa wa benki hiyo wakishuhudia nje ya mlango wa kuingilia gerezani.
Fumbuka(wa pili kutoka kushoto) na maafisa wenzake wakiwa nje ya lango
Misaada ikiendelea kushushwa