Mauzo ya hisa DSE yapanda kwa asilimia 65, sasa yafika Bilioni 32.5
Mauzo
ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) katika kipindi cha wiki
iliyopita yameongeza kwa asilimia 65 kutoka Sh. Bilioni 19.6 na kufikia
bilioni 32.5.
Afisa
Masoko Mwandamizi wa DSE, Mary Kinabo wakati akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam, amesema kilichochangia mauzo hayo
kupanda ni ongezeko la uhitaji wa hisa kwa kampuni wanachama wa soko
hilo na wateja wanaohitaji kununua.
Amesema
idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zimepanda zaidi ya mara nne
kutoka milioni 2.4 na kufikia milioni 9 za kitanzania.
Hata
hivyo, Kinabo amesema kutokana na kushuka kwa bei kwenye kaunta za NMB
na ACA, mtaji wa soko la DSE, umeshuka kwa asilimia 0.41 kutoka trilioni
21.579 hadi 21.49 trilioni.
Pia amesema mtaji wa makampuni ya ndani umepanda kwa asilimia 0.36 kutoka trilioni 8.1 hadi trilioni 8.14.
Aidha,
Kinabo amesema Sekta ya viwanda imepanda kwa pointi 26.16, sekta ya
huduma za kibenki na kifedha imeshuka kwa alama 0.52 na sekta ya huduma
za kibiashara imeshuka kwa alama 4.19.