RC MARA AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI WA VYANDARUA VYENYE DAWA
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi amezindua zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa vinavyotolewa bure na Serikali kwa wananchi wa Halmashauri saba za Mkoa wa Mara huku akiwaonya watumishi watakaojihusisha na uuzaji wa Vyandarua hivyo kwa wnaanchi
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika Zahanati ya Guta, Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mhe. Mtambi amewataka wananchi waliojiandikisha kufuata vyandarua na kuvitumia kujikinga na mbu waenezao malaria.
Aidha, amewataka viongozi wa ngazi za Wilaya na Halmashauri kusimamia zoezi hilo liweze kufanyika vizuri katika maeneo yao.
Jumla ya vyandarua 117,851 vinatarajiwa kugawiwa kwa wananchi waliojiandikisha kutoka kaya 35,513 za Mkoa wa Mara na Halmashauri ambazo hazimo kwenye mpango huo ni Manispaa ya Musoma na Halmashauri ya Mji wa Bunda.





