KATIBU ITIKADI NA MAFUNZO ARUSHA ASHINDWA KUJIZUIA
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Saipulan Ramsey, amesema Serikali ya Awamu ya Sita haiwezi kupimwa kwa maneno au mitazamo ya watu, bali kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayowanufaisha wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Julai 21, 2026, ofisini kwake jijini Arusha, Ramsey amesema si sahihi kuhitimisha kuwa serikali haipendwi kutokana na matukio yanayotokea kwenye majukwaa ya burudani au mijadala ya mitandaoni. Amesisitiza kuwa kipimo halisi cha serikali ni matokeo ya kazi na huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Aidha, amewataka watumishi wa umma pamoja na viongozi wa CCM katika ngazi zote kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kuwahudumia wananchi ipasavyo, ili kuendelea kujenga imani ya wananchi kwa serikali.
