RC YAHYA AWASILI KAGERA K UANZA MAJUKUMU YAKE.



Na Mwandishi wetu  Kagera.

Mkuu wa mkoa Kagera  mpya Kanali Yahya Ramadhani Kido  tayari amewasili mkoani humo kuanza majukumu yake ya kuwatumikia wananchi.

Kanali Kido baada ya kuwasili uwanja wa ndege Bukoba leo hii Tarehe 11 Februari amepokelewa  na watumishi mbalimbali wa ofisi ya  mkoa sambamba na viongozi wa manispaa ya Bukoba akiwemo mkuu wa wilaya Bukoba Mhe Erasto Sima pamoja na wakuu wa  kamati za ulinzi na  usalama.

Mkuu wa  mkoa huyo aliteuliwa Tarehe 6 Februari 2026 na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akipokea nafasi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe  Fatma Mwassa

Powered by Blogger.