PSSSF WAKABIDHI MILIONI 361.5 UKARABATI NA KUWEKA VIFAA TIB A CHUMBA CHA UPASUAJI.

 



Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetoa zaidi ya Sh 361.5 Mil kwa ajili ya kukarabati na kuweka vifaa tiba katika chumba cha upasuaji cha Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Cancer Institute (ORCI) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jumatatu Februari 23, 2026 wakati wa hafla ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk Diwani Msemo, amesema hatua hiyo ni ya kihistoria kwani chumba hicho kilihitajika tangu mwaka 1996.
“Mlichofanya leo hii kimekuja kuleta majibu ya miaka 30 iliyopita,tunashukuru kwa kuungana na Serikali ya Dk Samia Suluhu Hassan kupeleka furaha kwa wananchi,” amesema Dk.Msemo.
Amesema, uwekezaji huo utaongeza ubora wa huduma za matibabu ya saratani nchini kwa kuwepo kwa chumba cha kisasa cha upasuaji pamoja na vifaa tiba vya kisasa.
Hatua hiyo itagusa.
moja kwa moja maisha ya wananchi, wakiwemo wastaafu na wanachama wa PSSSF.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama wa PSSSF, Omega Ngole, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Fortunatus Magambo, amesema uamuzi wa kutoa fedha hizo ulitokana na ziara ya awali iliyobaini kuwa taasisi hiyo haina chumba cha upasuaji kinachojitegemea kwa wagonjwa wa saratani.
Kati ya fedha hizo Sh. 197,027,956 zitatumika kukarabati chumba cha upasuaji, Sh. 164,491,270 zitatumika kununua vifaa tiba.
Ngole amesema PSSSF itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya afya kupitia sera yake ya uwekezaji kwa jamii (CSI) chini ya kaulimbiu ya #PSSSFKaribunaJamii.
Hatua hiyo inatarajiwa kunufaisha maelfu ya Watanzania wanaohitaji huduma za matibabu ya saratani nchini.
Powered by Blogger.