KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI.
Katikati aliyevalia kofia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Ayubu Makuruma
Kamati ya Fedha na Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, imefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo tofauti ya Halmashauri hiyo.
Ziara hiyo ilihusisha ukaguzi wa miradi ikiwemo ujenzi wa madarasa mawili na matundu sita ya vyoo katika shule ya Msingi Kambarage B, Ujenzi wa miundombinu ya maji, vyoo bora na usafi Zahanati ya Kebosongo, Ukamilishaji wa Mabomba mawili ya madarasa shule ya Msingi Burunga, Ukamilishaji wa maabara Ikoma Sekondari na Ujenzi wa matundu 20 ya vyoo shule ya Sekondari Robanda iliopo Kata ya Ikoma.
Miradi hiyo inatekelezwa kupitia vyanzo mbalimbali vya fedha, ambapo baadhi inatekelezwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri, huku mingine ikitekelezwa kwa fedha kutoka Serikali kuu, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha huduma za kijamii na kukuza uchumi wa wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Ayub Mwita Makuruma, amepongeza kwa kiwango kikubwa utendaji kazi wa Halmashauri, hususan katika usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha za umma na ubora wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha, Kamati imempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Maulid Madeni (PhD) pamoja na timu ya wataalamu kwa kuonesha uwajibikaji, nidhamu na weledi katika kusimamia miradi ya maendeleo, hatua inayochangia kuleta matokeo chanya kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
Kamati ya Fedha na Uongozi imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo na kusisitiza kuendelea kudumisha kasi, ubora na thamani ya fedha ili kuhakikisha miradi inawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa


.jpeg)