ISRAEL KUPIGA MARUFUKU MSF KUFANYA KAZI HUKO GAZA KWA KUKATAA KUTOA ORODHA YA WAFANYIKAZI WAKE

 


Israel inasema itapiga marufuku Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) kufanya kazi huko Gaza baada ya shirika la misaada la matibabu kukataa kukabidhi orodha ya wafanyikazi wake katika eneo hilo.

Serikali ya Israel ilikuwa imeamuru mashirika 37 kuwasilisha nyaraka kuhusu wafanyakazi wao wa ndani na wa kimataifa huko Gaza, wakidai baadhi katika MSF walikuwa na uhusiano na makundi yenye silaha Hamas na Islamic Jihad.

Shirika la hisani limekanusha vikali hili.

MSF ilitangaza siku ya Ijumaa kwamba haitashiriki orodha ya wafanyakazi wake wa Palestina na kimataifa na mamlaka ya Israel kwa kuwa haijapata "hakikisho la usalama wa wafanyakazi wetu".

Katika kujibu, Israel ilisema "inaelekea kusitisha shughuli" za MSF huko Gaza.

Wizara ya Israel ya Masuala ya Diaspora na Kupambana na Kupinga Uyahudi ilisema uamuzi huo ulifuatia "kushindwa kwa MSF kuwasilisha orodha za wafanyikazi wa ndani, hitaji linalotumika kwa mashirika yote ya kibinadamu yanayofanya kazi katika eneo hilo".

Mnamo tarehe 30 Disemba, Israel ilitangaza kuwa ingefuta leseni za mashirika 37 ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi huko Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, ikisema kuwa yameshindwa kukidhi mahitaji mapya ya usajili,

@PICHA NA Bbc swahili 

Powered by Blogger.