370 MILIONI ZA GRUMETI RESERVES LIMITED NA TAWA ZA PELEKA TABASAMU SERENGETI NA BUNDA


 Shilingi Milioni 370   zimetumika kununua vifaa Tiba na vifaa vya Elimu ikiwemo madawati zaidi ya elf Tatu pamoja na computer ,katika shule za msingi wilaya ya Serengeti na Bunda mkoani Mara, ambazo zimetolewa na Shirika la Grumet Reserves Limited kwa kushirikiana na Tawa, huku wananchi wakionywa kuacha kujijusisha na shughuli za Ujangili kwenye maeneo ya Uhifadhi kwani kufanya hivyo nikuzipoteza rasilimali hizo ambazo nimhimu kwa Taifa.

Vifaa hivyo vimetolewa kufutia jamii kushiriki katika uhifadhi  wa mazingira na wanayamapori katika mapori ya akiba ya ikorongo na Grumeti kupitia mfuko wa uhifadhi mahiri SWICA na sasa shule za msingi katika wilaya ya Serengeti pamoja na Bunda  ambapo vitanda,madawati ,computer na UPC Aambazo zinapelekwa katika maeneo lengwa.

 

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyto vya elimu na Afya Mwenyekiti wa kamati ya Uhifadhi jamii mahiri kwanibaya ya Mkurugenzi Mkuu wa Grumeti Reserves LMited alisema msaada uliotolewa nipamoja na madawati 3,1014 ,vitanda 16 kwajaili ya kujifungulia ,Computer 19 pamoja na uwekeaji wa maji  kwa shule moja ya msingi.

“Tumetoa madawati 1,534 kwa wilaya ya Bunda  na 1,480 kwaajili ya wilaya ya Serengeti  vitanda 12 na vingine vine kwaajili ya wilaya ya serenegeti pamoja vifaa vya Tehama kwa wilaya ya zote”Alisema  Frida Mollel.

Kwa uapnde wake mkuu wa wilaya ya Serengeti Angelina Marco amesema matunda ya uhifadhi ya  yanamchango mkubwa katika maendeleo nchi huku akaiwataka wananchi kushiriki katika uhifadhi sambamba naye mkuu wa wilaya ya Bunda akawataka wananchi kuhakikisha wanaachana na vitendo vya ujangili katika maeneo yao.

 

Powered by Blogger.