OFISI YA MBUNGE MUSOMA VIJIJINI YA KABIDHI VITENDEA KAZI KWA VIONGOZI WA CHAMA.
![]() |
| Picha ni Viongozi wa Kata na Matawi mbalimbali wakikabidhiwa vifa. |
![]() |
| Sehemu ya viongozi wakiwa picha ya pamoja mara baaada ya kukabidhiwa vifaa hivyo. |
Na Fedson Masawa, Msaidizi wa Mbunge
Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya
Musoma Vijijini zimepokea vifaa (stationery) za ofisini kutoka kwa Mbunge wa
Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa ajili ya kuimarisha
utendaji kazi wa Ofisi hizo kama walivyowasilisha ombi lao hilo kwa Mbunge
huyo.
Wakipokea vifaa hivyo, Makatibu wa CCM kutoka
Kata 21 na Matawi 94 Musoma Vijijini wameshukuru kupatiwa vifaa hivyo na
kuahidi kukitumikia Chama chao kwa jitihada zote ili kuleta mafanikio
makubwa ndani na nje ya Chama hicho.
Miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa kwa makatibu hao ni pamoja na rimu za karatasi, mafaili, stempla, mashine za kutobolea karatasi, kalamu n.k
Ofisi ya Mbunge.




