MRADI WA UFUGAJI WA SAMAKI WAFIKIA HATUA NZURI MUSOMA VIJIJINI.




Picha hatua ulipofikia Mradi na shughuli ya uchimbaji ikiendelea.



Na James Francis, Msaidizi wa Mbunge
Utekelezaji wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki unaosimamiwa na Kikundi cha Nyanja Bwawa Samaki kilichopo Kijiji cha Nyang'oma, Kata ya Mugango upo katika hatua nzuri baada ya Kikundi hicho kufikia hatua za mwishoni za uchimbaji wa mabwawa hayo kwa ajili ya kufugia samaki.


Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge Mwenyekiti wa Kikundi hicho Ndugu Shida Mabeba, kwa niaba ya Wanakikundi wenzake amesema kuwa, wanatarajia kukamilisha hatua ya uchimbaji wa mabwawa ifikapo 5April 2018 ili kwenda hatua inayofuatia.


pia , Ndugu Mabeba alitoa shukrani zake kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo kwa kuchangia gharama za uchimbaji wa mabwawa hayo.
"Kwa niaba ya Wanakikundi wenzangu, napenda kutoa shukrani za pekee kwa Mbunge wetu kwa kutuwezesha kufanikisha hatua ya uchimbaji wa mabwawa," ameshukuru Ndugu Mabeba.

Aidha Mwenyekiti ameongezea kuwa, jukumu lao kubwa sasa, wao kama Wanakikundi ni kujituma kwa umoja wao kuhakikisha wanausimamia Mradi huo ili kuinua uchumi wa Wanakikundi na jamii inayouzunguka Mradi huo.


Ofisi ya Mbunge

Powered by Blogger.