Makeup Haya : KUTANA NA MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WAWILI WENYE BABA TOFAUTI
Katika hali ya kushangaza huko nchini
Uganda, wanaume wawili na watu wengine wamejikuta kwenye mshangao baada
ya kukuta wote wawili ni baba wazazi wa watoto wawili mapacha.
Inaelezwa kuwa wanaume hao waliingia kwenye mgogoro siku za hivi
karibuni kila mtu aking’ang’ania kuwa baba mzazi wa mapacha hao, na
ndipo walipoamua kwenda hospitali ili kupima kipimo cha DNA.
Hata hivyo matokeo ya daktari yalionesha kuwa wanaume hao wote wawili ni
baba halali wa mtoto mmoja wa mapacha hao, yaani kila mmoja ana mtoto
mmoja kati ya mapacha hao.
Inaeelezwa kuwa wanaume hao Joseph Baseka Sengendo, 25, na Patrick
Ssegane, 30, wamezaa na Rashida Nakabugo, ambapo Sengendo anatajwa kuwa
mume wa ndoa wa mwanamke huyo.
Wanaume hao wanasemekana kuwa ni ndugu.
