KARATU WAPUUZA AGIZO LA SERIKALI.

sipicha ya tukio husika.
NA EVA-SWEET MUSIBA(ARUSHA)
NAIBU Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi amesikitishwa kuona kuwa maagizo yanayotolewa na serikali yanapuuzwa, ikiwemo upimaji viwanja na makusanyo ya kodi za ardhi tangu mwaka jana walipoagizwa kufanya hivyo.
Akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Karatu, Mkoani Arusha katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo alisema kuwa ni uzembe wa hali ya juu kwa watumishi kutofatilia maagizo yanayotolewa na serikali hasa ukiangalia kuwa hata asilimia 30 ya makusanyo ya kodi za ardhi ambayo tayari ilishafutwa imejitokeza tena.
Suala jingine ni kuwepo kwa visingizio vya kutokukusanya kodi kuwa hakuna mtandao jambo ambalo si la kufumbia macho katika suala zima la makusanyo ya kodi ya mapato na kwamba mwaka wa jana walishingizia kuwa hawana moderm.
“Hakuna sekta yenye pesa nyingi kama hii, lakini mnaidharau, mmeshindwa hata kudai madeni ambayo wadau wengi wanadaiwa kodi, hatuwezi kuwa na watu ambao hawawezi kufanya kazi chagua nini cha kufanya yaani ni vitu vya ajabu sana, mwaka jana mlisema hamana moderm, mwaka huu mtandao ni tatizo, mara bando, halmashauri inashindwa kununua bando, eh… Mkurugenzi” Alihamaki Mabula.
Alisema halmashauri zinatakiwa kufanya zoezi la urasimishaji kwa maeneo ambayo hayakupangwa na kupima ili kuzuia miji kuharibika kwa ujenzi holela.
Aliagiza pia kuwa kila robo ya mwaka itoe taarifa za makusanyo ya kodi(maduhuri), kwani taasisi nyingi zinadaiwa ikiwemo, Tanesco, kampuni ya bia ya Tanzania Breweries na wengine wengi ambao wamekalia mamilioni ya serikali.
Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri, Kaimu Mkurugenzi wa Mtendaji wa halmashaurihiyo, Dk. Eliphas Mollel alisema kuwa kwa kipindi cha Julai 2017 hadi februari 2018 kitengo cha upimaji wa ardhi kimeweza kuwapimia wananchi jumla ya viwanja 924 vilivyopo Karatu mjini katika Block “J” na “F” na kati ya ya hivyo, viwanja 154 vimeishajaliwa na Wizara ambapo jumla ya viwanja 770 vinaandaliwa.
Aliongeza kuwa kwa upande wa taasisi kitengo hicho kimeweza kupima taasisi za umma zipatazo 323 katika vijiji 58 kwa kutumia sheria Na.5 ya ardhi ambapo upimaji huo umejumuisha shule za sekondari 20, kati ya 30, shule za msingi 72 kati ya 106,zahanati na vituo vya afya vyote 32 zimepimwa, mashamba 56 na maeneo mengine ya majosho,viwanja vya mpira na ofisi za vijiji.
Aidha Naibu Waziri huyo ameipongeza halmashauri hiyo kwa kufanya upimaji katika taasisi kwani migogoro mingi ya ardhi huwa inakuwa maeneo hayo.