HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MARA ,YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MADAKTARI BINGWA.
Sipicha ya tukio husika
HOSPITALI ya rufaa ya Mkoa wa Mara iliyopo katika Manispaa ya Musoma inakabiliwa na upungufu wa Madaktari bingwa 19 pamoja na wauguzi 91, hali inayosababisha kuzidiwa majukumu kwa watumishi waliopo na kupelekea kupunguza shauku ya kufanya kazi.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Joachim Eyembe aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mwishoni wakati wa uzinduzi wa duka la dawa la hospitali hiyo, alisema kwa ujumla hospitali hiyo ina tatizo la ukosefu wa watumishi wenye sifa 378 sawa asilimia 55.3 ya wanaohitajika.
Alisema katika kukabiliana na changamoto hiyo hatua mbalimbali zilifanywa na uongozi wa hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na wizara ya afya na Tamisemi juu ya uwepo wa upungufu huo.
"Tuna madaktari wa upasuaji wawili na wauguzi 67 tu, pia tuna uhaba wa madaktari wasaidizi, wateknolojia ya maabara pamoja na wateknolojia Madawa,ili kupunguza tatizo tumeruhusu madaktari ambao bado hawako katika ajira kujitolea hii ni pamoja na watumishi wa kada nyingine ikiwemo wafamasia" alisema Eyembe.
Mganga mkuu wa hospitali hiyo Francis Mwanisi alisema
Malengo ya kuanzishwa kwa duka la hospitali hiyo, ni kutekeleza maelekezo ya serikali ya kuwepo kwa duka la Dawa kila hospitali ili kuondoa usumbufu kwa wagonjwa kwenda kutafuta Dawa nje zinapokosekana Kwenye dirisha la Dawa.
"Hospitali iliazimia kufungua duka la Dawa ili dawa na vifaa Tiba vipatikane kwa muda wote, mchakato wa kuanzisha duka hili ulianza septemba 2017 na kuanza kutoa huduma januari 18 mwaka huu kwa mkopo wa dawa toka MSD wa shilingi 206,936,758 lakini hadi sasa tumepokea mkopo wa dawa zenye thamani ya shilingi 182,657,367" alisema Dkt Mwanisi.Kwa upande wake mgeni rasmi mkuu wa mkoa Adam Malima alifarijika na kujituma uongozi wa hospitali hiyo kwa hatua walizopiga katika kuboresha huduma, alisema ataenda kuongea na uongozi wa juu wa wizara ya afya na kuomba bajeti ya mwaka huu iweze pia kuboresha suala la uhaba wa watumishi
"Nimeona kuna upungufu mkubwa wa watumishi hasa madaktari tumeubaliana nitaenda kuongea na wizara husika ili waangalie namna ya kuboresha changamoto hiyo ya wahudumu na wafanyakazi wengine ili kuongeza upatikanaji wa huduma na kuwapa wepesi wafanyakazi waliopo"
Mwisho.