MAAMBUKIZI MAPYA YA UKOMA YATAFUNA MIKOA 10, TANZANIA
Serikali imesema ugonjwa wa ukoma bado unaendelea kuwa tatizo huku ikizitaja wilaya 20 na mikoa 10 inayokabiliwa na maambukizi mapya ya ugonjwa wa huo.
Akizungumza na wanahabari kuhusu maadhimisho ya siku ya ukoma duniani yanayofanyika Januari 28 kila mwaka, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania miongoni mwa nchi 22 zenye wagonjwa wengi wa ukoma duniani.
Amesema kwa mujibu wa takwimu za Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma za mwaka 2016, zinaonyesha idadi ya wagonjwa wapya 2,047 wa ukoma waligunduliwa ambayo ni sawa na watu 4 kwa watu 100,000.
Ameeleza kuwa, tangu mwaka 2007 hadi 2017 takwimu zinaonyesha watoto 1,456 waligunduliwa na kutibiwa ukoma, ambao watoto 73 kati yao waligundulika kupata ulemavu wa kudumu kutokana na kukatika baadhi ya viungo vyao.
Dkt. Ndugulile ametoa wito kwa wananchi watakao ona dalili za ukoma ambazo ni pamoja na kutokwa na mabaka kwenye ngozi, uvimbe na maumivu kwenye mishipa ya fahamu na ganzi kwenye mikono, kujitokeza hospitali kupata matibabu kwa kuwa hutolewa bure, badala ya kuendekeza Imani potofu kwamba ugonjwa huo wa kurithi au kulogwa.
Mikoa inayokabiliwa na ugonjwa wa Ukoma ni, Lindi, Mtwara, Rukwa, Pwani, Morogoro, Geita, Tanga, Tabora, Dodoma na Kigoma. Kwa upande wa Wilaya ni Kilombero, Mafia, Pangani, Mvomero, na Masasi Mjini.