WATU 34 WATHIBITIKA KUFA KWENYE AJALI NCHINI KENYA

Image result for PICHA AJALI YA BASI KENYA
Sipicha ya tukio husikaA

Habari kutoka Kenya zinasema watu 34 wamefariki na wengine 16 kujeruhiwa kwenye ajali ya barabarani baada ya basi moja la abiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo katika maeneo ya barabara ya Sachangwan/Salgae takribani Kilometa 200 kutoka mji mkuu Nairobi.

Afisa mkuu wa idara ya polisi kitengo cha trafiki maeneo ya Bonde la Ufa, Zero Arome amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tisa alfajiri kwenye barabara kuu ya kutoka Nakuru kuelekea Eldoret Mashariki mwa Kenya.

Majeruhi wamepelekwa katika hospitali za Nakuru Level Five na ile ya Molo sub-Country kwa ajili ya matibabu zaidi, huku miili ya marehemu ikipelekwa kwenye hospital ya Nakuru Level Five kwaajili ya ndugu kwenda kuwatambua wapendwa wao.
Powered by Blogger.