HOSPITALI ZATAKIWA KUPATA WATAALAMU WA DAWA ZA USINGIZI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amesema vituo vyote 211 vinavyoongezewa miundombinu ya Afya vinahitaji wataalam wa kutoa Dawa za Usingizi ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa watakaofikishwa katika chumba cha Upasuaji pamoja na Wodi ya Kinamama.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya Kikazi Wilayani Mpwapwa na kukagua miradi ya maendeleo iliyompelekea kufika katika ujenzi wa miundombinu ya Afya inayojengwa katika Kituo cha Afya Mima.

Akiwa kituoni hapo alisema ameridhishwa na ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo hii ya awamu ya kwanza itakamilika mapema Mwezi Januari 2018 lakini anaona uhitaji wa wataalam wa kutoa Dawa za Usingizi ambao watatoa huduma hizo wakati wa upasuaji na huduma nyingine muhimu.
“Nataka vituo hivi vinapokamilika vianze kufanya kazi mara moja na sio zianze sababu mara wataalamu Fulani hakuna hiki bado sitapenda kusikia hayo ni vyema kwa sasa kila Mkurugenzi wa halmashauri ahakikishe anabainisha wataalam angalau wawili ambao watakwenda kupata mafunzo mafupi ya utoaji wa Dawa hiyo ya Usingizi wakati wa Upasuji”.

Mpaka sasa nimeridhishwa kabisa na kasi ya Ujenzi wa vituo hivi vya Afya na kwa sababu vifaa Tiba pia tunapata kutoka Bohari Kuu ya Dawa sasa kwa pamoja tuangalie maeneo mengine ambayo yataenda sambamba na utoaji wa huduma katika vituo hivi kama wataalamu hawa ambao kwa Takwimu zilizopo kwa sasa bado ni wachache na baada ya ukamilishwaji wa vituo hivi Uhitaji Utakua Mkubwa zaidi alisema Waziri Jafo.

Awali akitoa Taarifa ya Ujenzi Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Space East Africa iliyopewa Kazi ya Kujenga Kituo cha Afya Mima Gaston Francis amesema kampuni hiyo hujenga kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa iitwayo “Pre-Fabricated Material” ambayo ni nafuu zaidi na ina ubora wa hali ya juu hivyo kwa gharama hiyo ya Mil 500 watajengwa majengo saba huku yakiwa na thamani zote zinazohitajika “Full furnished”.

Aina hii ya Teknolojia hutumika sana maeneo yenye vimbunga, upepo Mkali na Dhoruba mbalimbali na kwa sababu eneo hili la Mima linaathiriwa sana na wadudu Material hii tunayotumia itaenda kuwa suluhisho la kudumu la wadudu hao kwa sababu hawataweza kuathiri hata eneo moja na majengo tutakayojenga na ubora wa material hizi tunazotumia zinadumu kwa Zaidi ya miaka sabini alisema Francis.

Awali katika ziara yake Waziri Jafo alianza kwa kutembelea ujenzi wa barabara ya Lami ( Km 1 ) iliyojengwa kuanza NMB Mpwapwa mpaka Stendi ya Mpwapwa, kukagua Mradi wa Maji Mima pamoja na kuzungumza na wananchi wa Mima kwenye Mkutano wa hadhara
Powered by Blogger.