MBUNGE WA MUSOMA MJINI AWATAKA WANANCHI KUMUUNGA MKONO KUCHANGIA MAENDELEO



 Image result for PICHA VEDASTUS MATHAYO MBUNGE WA MUSOMA
WAKAZI wa kata ya Nyakato wamelalamikia ubovu wa barabara za mitaa zilizopo katika kata hiyo ambazo zimekuwa zikileta adha kubwa kwa wananchi hali inayohatarisha usalama wa maisha yao.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara wa kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka miwili, ulioitishwa na Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya, Magiri Maregesi na Mbunge wa Jimbo hilo, Vedastus Mathayo katika viwanja vya ofisi ya CCM Kata hiyo, Jane John alisema kuwa barabara hiyo ya mtaa wa Bondeni imekuwa ikileta adha kubwa hasa wakati wa matatizo na hadi kupelelea huduma kutokidhi vyema.

Alisema kuwa miezi kadhaa iliyopita gari la kuzimia moto lilishindwa kupita eneo hilo na kusababisha nyumba ya kulala wageni iitwayo Jumba la Dhahabu kuteketea huku maisha ya wakazi wa eneo hilo ikiwa hatarini.

Jitihada kutoka kwa wananchi kwa kata hiyo waliokuwa hapo ndizo zilizozaa matunda,huku mali ya nyumba hiyo yenye thamani ya zaidi ya Milioni 15 ikiteketea.

Aidha ameomba uongozi wa Manispaa waweze kushughulikia barabara hizo ili wakazi wa eneo hilo waweze kupita kwa magari, kuliko hivi sasa ambavyo magari hayapiti katika eneo hilo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mwenyekiti wa Wilaya ya Musoma, Magiri Maregesi alimwagiza Mkurugezi wa Manispaa hiyo, Fidelica Muyovella kupitia afisa elimu wa Wilaya kuhakikisha shule ya Nyakato A,B,C na Msangi zinaboreshwa na si kusajiri shule mpya kwani ni upoteza ni wa fedha za Serikali.

Shule ya Msingi Nyakato A,B,C na Capt.Msangi ina jumla ya shule saba, zote zikiwa katika eneo moja zikiwa na wakuu wa Shule wapatao 7, wakuu wa shule wasaidizi wapatao 7 huku shule ya Capt. Msangi ikiwa haijapata usajili kutokana na kutokuwa na vyoo ambapo katika eneo la shule hizo panajengwa shule nyingine mpya yenye madarasa mawili iitwayo maziwa.

Naye Mbunge wa jimbo hilo, Vedastus Mathayo aliwataka wananchi kuchangia katika kukamilisha vyumba vya madarasa ambapo yeye binafsi atatoa mabati na madawati.
Powered by Blogger.