HILI HAPA OMBI LA KIKUNDI CHA ULINZI SHIRIKISHI NYAKATO KWA SANANE;



MAKALIBLOG; MARA
Vijana wanao jihusisha na ulinzi shirikishi katika eneo la kwa sanane katika manispaa ya musoma wameiomba serikali na wahusika waulinzi kuwasaidia vifaa ikiwemo viatu na makoti pamoja na vitambulisho kwani vijana hao wanaingia kulinda wakiwa wamevaa kandambili.

Makaliblog ilizungumza na kaimu kamanda na kamanda wa wa kikosi hicho cha ulinzi bwana masumbuko juma alisema kwa sasa wananchangamoto kubwa ya vitendea kazi kwani wanaingia na kandambili kufanya shughuli zao jambo ambalo nihatari kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Masumbuko alilitaka jeshi la polisi mkoani Mara kuwasaidia vifaa angalau viatu nakuondokana na adha ambayo wanaipata sasa ya kuvaa kandambili na kuingia nazo lindo ambapo haiwapi uhuru wa kufanya kazi kwa weredi kwani wanafanya katika mazingira magumu.

Naye seseme ambaye nikijana katika kikosi hicho ambaye pia yeye nimpelelezi wa matukio katika kikosi hicho alisema mpaka sasa wanapo wakamata watuhumiwa inawalazimu kuwafunga kwa kamba badala ya pingu.

Hivyo nivyema jeshi la polisi kupitia kwa kamanda wa polis mkoa likasikia kilio chetu japo wamekuwa wakitusaidia gari tunapo hitahiji kwa haraka shida yetu kubwa nivifaa.

nivyema wakawasaidiwa vifaa hivyo wakafanya kazi kwa uhuru zaidi.

“kamanda akisikia kilio chetu atusaidie ambapo mpaka sasa wananchi wenzetu ndio wanatuhudumia polisi wao hawajatuacha tukiomba msaada wanatuletea gari mapema ila hatuna vitendea kazi sasa”alisema seseme.

Kwa upande wake mzee Ramadahini mtundu ambaye ndiye mwanzilishi wa kikosi hicho nimstaafu wakikosi cha ulinzi alisema toka hajastafu waliomba vifaa na hawakupewa hadi anastafu ulinzi ambapo sasa ameitaka serikali kutowatelekeza vijana wanaojitokeza kwa ulinzi.

Awali eneo la Nyakato musoma nikati ya eneo ambalo lilikuwa linaokopeka kwa vibaka lakini sasa nyakato pako salama na hakuna tena matukio mabaya kama ilivokuwa ikilipotiwa awali.

Kundi hilo toka lianzishwe limesaidia kuondoa uhalifu kwa asilimia kubwa katika eneo hilo lililokuwa sugu nakukithiri kwa uharifu katika eneo hilo la nyakato.

Aidha Gerad obagi ambaye nikamanda wa kikosi hicho alisema nimda mrefu wamefanya ufatiliaji wa ngazi zote lakini hajapata majibu au mrejesho wowte wamaombi yao ya vifaa vya ulizi.

walisema toka akiwa kamanda wa polis wa mkoa wa mara Ramdhani Ng'azi aliwahi kuwapa pea za viatu ambazo sasa zimekwisha na wala hazitumiki natoka kipindi hicho cha kamanda rama hawajawahi kupewa tena.
Powered by Blogger.