AJIBU ATUMA SALAM MSIMBAZI


MOTO wa Ibrahim Ajib umezidi kuwaka baada ya leo kutupia mabao mawili katika mchezo dhidi ya Stand United na kufikisha matano ikiwa ni matatu tu nyuma ya kinara Emmanuel Okwi mwenye mabao manane.

Yanga wameibamiza Stand mabao 4-0 kwenye uwanja wa CCM Kambarage huku mabao mengine mawili yakifungwa na Pius Buswita na Obrey Chirwa.

Mabao mawili ya Ajib leo yameamsha ‘mzuka’ kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu baada ya kupunguza tofauti ya mabao kati ya anayeongoza na anayemfuatia na kubakia matatu pekee.

Geofrey Mwashiuya akiwatoka walinzi wa Stand United

Simba na Yanga zitakutana kwenye mchezo wa mzunguko wa nane wa ligi kuu hapo Oktoba 28 ikiwa ni nafasi kwa Okwi na Ajib kuendelea kuonyeshana kazi kwenye kucheka na nyavu.

Baada ya mechi ya leo, Yanga watasafiri kwenda kisiwani Pemba kwa ajili ya kambi maalum kuelekea mchezo huo huku Simba wenyewe wakitarajiwa kuondoka kesho kwenda mjini Zanzibar.
Powered by Blogger.