VIDEO.MAKALIBLOG;SAFARI YA VIWANDA MKOANI MARA YA IVA,MTIZAME DC wa MUSOMA DKT. VICENT ANNEY ALICHOKISEMA;
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt Vicent Anney akizungumzia fursa zilizoko katika mkoa wa mara namipango iliyopo sasa yakufufua viwanda vilivyopo mkoani humo nakuongeza vingine.
Profesa Haidari Amani ambae nimtafiti mwandamizi na mtaalamu wa uchumi ambae alishiriki katika mkutano huo wawadau wa maendeleo kutoka sekta binafsi
Na MAKALIBLOG; Mara
WANANCHI mkoani Mara wametakiwa kufanya shughuli za kilimo kwa nguvu zote ikiwa ni pamoja na kuboresha,kuongeza thamani ya mazao yao ili kuweza kupata masoko kwa faida ya maendeleo binafsi na kukuza pato la taifa.
Mwito huo umetolewa juzi na Mkuu wa wilaya ya Musoma Vicent Naano katika mkutano wake na wadau wa maendeleo kutoka sekta binafsi uliokuwa umewashirikisha wataalamu mbalimbali wa uchumi.
Mkutano huo uliwataka washiriki kuzitambua fursa mbalimbali za uwekezaji hasa katika viwanda zilizopo mkoani humo na kuzichangamkia kwa haraka jambo lililoelezwa na mkuu huyo wa wilaya kuwa kilimo kina nafasi kubwa katika uanzishwaji wa viwanda.
"Lengo letu ni kwamba sasa wananchi na wafanyabiashara wajenge viwanda vya kusindika mazao katika maeneo ya mpakani mfano wilaya ya Tarime inapata changamoto ya njia za panya za wafanyabiashara" alisema.
Alisema serikali mkoani hapa imeazimia kujenga viwanda viwili vya kuzalisha kilimo cha alizeti na Pamba vilevile imejiwekea mkakati wa kujenga centre ya biashara ya mazao itakayo hifadhi mazao ya kusindika kama alizeti,mahindi na mtama.
Kwa upande wake mtafiti mwandamizi mshiriki ambaye ni mtaalamu wa uchumi Haidari Amani alisema wamebaini kuwa mkoa huo una fursa nyingi za uwekezaji hasa upande wa kilimo cha pamba.
"Uwekezaji katika viwanda vya pamba zipo za aina nyingi mfani kusuka nyuzi hizo ni fursa nyingi eneo lingine ni kuboresha thamani ya mazao ya kilimo cha matunda, mbogamboga maziwa wana fursa hizo pia wanaweza kujenga kiwanda cha kuzalisha simenti katika wilaya ya Serengeti kwasababu wana gypsum" alisema Amani.
Mda wa maendeleo kutoka sekta binafsi mshirki katika mkutano huo Boniphace Ndengo alisema hayo yote yatawezekana endapo serikali itatengeneza mkakati wa kuwatambua wajasiriamali.
"Ili tuweze kufikia malengo ya uwekezaji was fursa za viwanda inabidi tutengeneze namna ya kuwapata wajasiriamali kwa kuwasaidia mtaji,elimu na kuwahamasisha kufikia suala la kuwekeza katika viwanda kwa maendeleo ya taifa"alisema Ndengo.