WANANCHI WAAHIDI KUMUUNGA MKONO MWENYEKITI WAO WA SERIKALI YA MTAA;

Na Makaliblog, Mara.
Wananchi wamtaa wa Nyabisare kata ya Bweri katika manispaa ya musoma mkoani Mara wameshangazwa kuwepo kwa taarifa za uzushi zakumkataa mwenyekiti wa mtaa huo nakusema kuwa sizakweli nazinasambazwa na watu ambao wanapinga jitihada za maendeleo zinazofanywa na mwenyekiti huyo.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara katika shule ya sekondari iringo wananchi hao walisema kuwa kumekuwepo nataarifa zinazomhusu mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bwana Samweli wegoro kukataliwa na wananchi wamtaa huo.
Mmoja wawakazi hao akichangia katika kikao hicho ambae hakutaka jina lake litajwe alisema watu ambao wanasambaza taarifa hizo nakuwatumia baadhi ya viongozi nikutokana na kujituma kwa mwenyekiti huo katika utendaji kazi wake.
‘Mwenyekii tunaakuamini sana wewe umekuwa mkombozi wetu katika mtaa huu umetusaidia mpaka sasa tulikuwa hatuna barabara lakini kwa jitihada zako tunabarabara sasa’’alisema mwananchi huyo ambae hakutaka jina lake litajwe.
Pamoja natuhuma hizo wananchi hao wamesema bado wananchngamoto nying ikiwemo ukosefu wa maji katika eneo lote sikwa mtaa bali nikijiji cha nyabisare ambapo hawana maji ambapo inawadhimu kutembe umbali mrefu.
Naye Bwana juma sospeter alisema kuwa shule pia imekuwachangamoto kubwa katika kijiji hicho ambapo sasa wazazi inawabidi wakati mwingine kuwasikiza watoto shule jambo ambalo linapunguza uzalishaji.
Juma alisema watoto wanabakwa nahata kulawitiwa kwa sababu ya umbali kwani wapo wengine ambao wamekuwa wakiamka asbuh na wengine kuchelewa vipindi hivyo kuogopa kuingia darasani.
‘Kiukweli shule nichangamoto sana serikali yetu ingetusikiliza wanayabisare kwani tunachagamoto kubwa sana kwani wengine wanapotea wakati wakurudi hasa wanaonza dara la kwanza.’’alisema juma
Aidha mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bwana Samweli wegoro alikiri kuwepo kwa kero hiyo ya umbali wa shule kwani alisema anapata kesi nyigi za watoto kupotea ambapo sasa watoto wengwamekuwa wakipelekwa kwake wanaopotea.
Samweli alizungumzia pia kuhusiana na kashfa inayomhusu yeye yakukataliwa nawananchia nakusema kuwa alishangazwa na taarifa zilizotolewa zikisema kuwa amekataliwa na wananchi wa mtaa wake kitendo ambacho wengi walifikiri atajihudhuru katika mkutano wake nawananchi..
Wananchi wengi waliokuwa wamehudhuria kikao hicho walikuwa wamepanga endapo angejihudhuru baadhi yao walikuwa wamepanga kwenda kuchoma nyumba zake